Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Kudirect video basi, nitabaki kama mwalimu kwa vijana – Adam Juma

Mtayarishaji mkongwe wa video za muziki nchini, Adam Juma amesema kwa sasa hana mpango wa kufanya video za muziki, kama ambavyo alivyokuwa akifanya awali.

Adam Juma amesema kwa sasa hivi atafanya kazi iwapo ataona msaada wake unahitajika, pamoja na kuwapa elimu vijana amabo wanaingia kwenye taaluma hiyo.

“Kwa mimi sina mpango kama kuna mtu ana kazi yake nzuri naweza nikamsaidia, naweza nikashiriki hapa na pale labda kwenye kufundisha, mimi nimefanya mengi nimekaa takribani miaka 14 kwenye tasnia,” Adam Juma alikiambia kipindi cha Planet Bongo ya EA Radio. 
“Hivyo siwezi sema nataka kurudi, nitafanya kazi kwa mtu ambaye anajisikia anataka kufanya kazi kama kusaidia tu, lakini siyo kwa nia ya kutaka kufanya biashara”,
Adam Juma aliendelea kusema kwamba anaamini vijana wa sasa wanafanya kazi nzuri na kuendeleza pale alipoachia, hivyo anakaa pembeni kuwaachia wafanye kazi hizo.