Coutinho aachwa kwenye kikosi cha Liverpool dhidi ya Hoffenheim leo
Kiungo wa Liverpool, Philippe Countihno
ameachwa nje ya kikosi cha timu hiyo kitakachoshiriki mechi ya kwanza ya
michuano ya kufuzu kwa hatua ya makundi ya ligi ya klabu bingwa Ulaya
dhidi ya Hoffenheim leo.
Kiungo huyo wa kati, mwenye umri wa miaka
25, aliwasilisha ombi lake la uhamisho wiki iliyopita, siku chache
baada ya klabu hiyo kukataa euro milioni 100 (£90m) kutoka Barcelona.
Countinho alikosa mechi ya ufunguzi siku ya Jumamosi katika ligi dhidi ya Watford kutokana na jeraha la mgongo.
Barca wamekuwa na matamanio ya kumpata
Coutinho baada ya kumuuza Neymar kwa klabu ya Paris St-Germain kwa kima
kilichovunja rekodi ya dunia cha pauni milioni 200.
Coutinho alisaini mkataba wa miaka mitano mwezi Januari, ambao haukujumuisha kipengee cha kuondoka kwake.
Liverpool wataanza kampeini yao ya Ulaya
na hatua ya kwanza ya muondoano katika uwanja wa Rhein-Neckar-Arena
nchini Ujerumani na mechi ya amrudiano itakuwa Anfield siku ya Jumatano
tarehe 23 mwezi Agosti.
Kikosi cha Liverpool: Alexander-Arnold,
Moreno, Lovren, Milner, Wijnaldum, Henderson, Can, Mane, Salah, Firmino,
Kent, Solanke, Origi, Gomez, Klavan, Flanagan, Robertson, Matip,
Grujic, Mignolet, Karius na Ward.