DONE DEAL:£75m, miaka 24, mabao 25 Lukaku ni usajili usio na shaka kwa United
Mwaka 2014 alikuwa ni kocha Jose Mourinho ndiye alihitimisha uhusiano
wa Chelsea na Lukaku baada ya kocha huyo kumuondoa Lukaku toka The
Blues akisema bado hakuwa hatari lakini kuanzia hapo Lukaku kiwango
chake kikawa kinakua.
Sasa miaka mitatu imepita toka Mourinho amuuze Lukaku na sasa
anamnunua kwa kiwango kikubwa sana cha pesa zaidi ya £75m na anamnunua
katika kipindi ambacho kwa hakika anahitaji mtu aina ya Lukaku kuja
kuokoa jahazi la United.
Msimu uliopita alikuwepo Zlatan Ibrahimovich ambaye kiuchezaji ana
tofauti na Lukaku kwani Zlatan alikuwa akisimama tu karibia na goli ili
kumalizia mipira inayokuja lakini Zlatan hakukidhi kwa 100% kilichokuwa
kikitarajiwa na United toka kwake.
Pamoja na kufunga mabao mengi lakini Zlatan pia alipoteza nafasi
nyingi, United walihitaji mshambuliaji na sio tu mshambuliaji walihitaji
mshambuliaji mwenye vitu vingi katika miguu yake kama ilivyokuwa kwa
Wayne Rooney alipokuwa kijana mdogo.
Hakuna ubishi kuhusu uwezo wa Lukaku, ni mshambuliaji ambaye ana kila
kitu ambacho mshambuliaji anapaswa kuwa nacho,anakimbia,ana skills na
ni muuaji wa nyavu, ni aina ya washambuliaji wanaoweza kukupa matokeo
katika nyakati ngumu.
Msimu uliopita alifunga mabao 25 na uzuri mabao hayo alifunga 7 kwa
mguu wa kulia na 12 kwa kushoto na kumfanya awe kinara wa kufunga kwa
guu la kushoto kitu kinachoonesha uwiano mzuri wa miguu yake na huku
mabao 6 akifunga kwa kichwa, ni dhahiri Lukaku anatumia vyema kila
kiungo kucheka na nyavu.
Ligi ya Epl ni ngumu na kwa mtu aliye chini ya umri wa miaka 25 kama
Lukaku ni jambo kubwa sana kufunga mabao zaidi ya 10 katika misimu
mitano mfululizo na hii inawapa United matumaini kwamba hawawezi kosa
mabao “double figure 10+” toka kwake.
Kucheza mbele ya Juan Mata, Mkhitaryan na Paul Pogba hakika inaweza
kuwa kilio kwa timu pinzani, aina za movements za Lukaku anapokuwa
uwanjani huwa zinawasumbua sana mabeki na uwepo wa viungo waliopo
Manchester United inaweza kuzidisha uhatari wa Lukaku.
Kutokana na umri wa Romelu Lukaku wa miaka 24
na uwezo wake wa kufunga nadhani dau lake ni sahihi kabisa na halina
mashaka hata kidogo kama linavyozungumziwa, kwa mshambuliaji ambaye kila
msimu anafunga mabao zaidi ya 10 na bado ni kijana mdogo £75m ni sahihi
kabisa haswa katika soka hili la pesa.