Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Agizo la RC Gambo kwa BAKWATA juu ya kucheza Kareti Msikitini

                                                         
                                                               (Rc Mrisho Gambo)
June 17, 2018 Nakusogezea story kumhusu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambapo amelitaka Baraza Kuu la Waislamu Arusha kukemea tabia ya baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam kucheza mchezo wa kareti misikitini na kusisitiza kuwa tabia hizo haifai
Gambo ametoa tamko hili baada ya kumalizika kwa ibada ya sikukuu ya Eid iliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri na kuwataka BAKWATA kukemea tabia hiyo.
Amesema kuwa tabia ya baadhi ya misikiti kufundisha waumini wake mchezo wa kareti ndani ya misikiti haifai na inapaswa kukemewa.
“Baadhi ya misikiti kufundisha karate haifai naomba niwapongeze BAKWATA kwa kukemea tabia hii na ninawaomba muendelee kulisimamia hili,” RC Gambo