Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema
serikali itawafikisha Mahakamani na kuwafutia hati ya umiliki wananchi
wote wanaomiliki ardhi ambao wamekuwa hawalipi kodi ya ardhi.
Waziri Lukuvi ametoa kauli hiyo leo Mei 29, 2018 Bungeni Jijini Dodoma
kwenye kikao cha 37 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya
Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/219 na kusema katika mwaka huu wa
fedha ambao unaishia mwezi Juni Wizara ya Ardhiilipanga kukusanya
Bilioni 112.5 vinavyotokana na vyanzo vya mapato ya kodi, ada na tozo
mbalimbali za ardhi lakini hadi Mei 15 wizara imeshakusanya Bilioni 78.9
sawa na asilimia 70 ya lengo lililokusudiwa.
"Natoa onyo kwa wadaiwa sugu wote wasiolipa kodi ya pango la ardhi
kwamba serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni
pamoja na kuwafikisha mahakamani, kuitaifisha mali zao ili kufidia
kiwango cha kodi wanachodaiwa au kufutiwa hati miliki", amesema Lukuvi.
Pamoja na hayo, Waziri Lukuvi ameendelea kwa kusema "kwa hiyo natoa wito
kwa wote wanaomiliki ardhi kisheria wakumbuke kulipa kwa mujibu wa
sheria".
Kwa upande mwingine, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi amesema bado kuna muitikio mdogo wa wananchi kumilikishwa
ardhi hususan katika maeneo ya urasimishaji ambayo yapo skwakta.
Serikali kuwafikisha Mahakamani na kuwafutia hati ya umiliki ardhi Wananchi hawa
Reviewed by mwabusila
on
5/29/2018 05:21:00 PM
Rating: 5