P – Funk akirudi rasmi kwenye muziki moto utawaka – Mr Ttouch
Mtayarishaji wa muziki ambaye anafanya vizuri kwa sasa, Mr Ttouch kutoka Touchz Sounds, hivi karibuni alimtembelea mtayarishaji mkongwe wa muziki P-Funk Majani kutoka Bongo Record na kupiga naye stori kuhusu tasnia ya muziki.
Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii, Mr Ttouch amedai alimtembelea producer
huyo kwaajili ya kumtakia hali kwa kuwa ni mtayarishaji mkongwe ambaye
anazifuatilia kazi zake kwa muda mrefu.
“P Funk nilimtembelea kumtakia hali tu kwa sababu ni producer ambaye
namfuatilia sana toka zamani, kwahiyo hakuna chochote kinachoendeleza
kati yetu,” alisema Ttouch. “Binafsi ukimya wa P-Funk naona kama kuna
kitu tunakikosa kwenye game, P-Funk ni mtu mwingine kwenye muziki naona
kama kweli angekuwa anaendelea kufanya project kama zamani game ya
muziki ingechangamka,”
Touch alisema bado hajapata nafasi ya kufanya kazi ya pamoja na mkongwe huyo.