Header Ads

PropellerAds

Breaking News

VIONGOZI WA DINI WAMPONGEZA KAMANDA SIRRO KWA KUTEULIWA IGP


IGP SIRRO
Viongozi wa Dini hapa nchini wamempongeza Kamanda Saimon Sirro kwa kuteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).Pongezi hizo zimetolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa jamii ya dini zote, Askofu William Mwamalanga kwa niaba ya viongozi wa dini.Katika mahojiano maalum, Kiongozi huyo wa dini amemuelezea IGP Sirro kuwa ni mchapakazi na mtu makini katika utendaji wake wa kazi.
“IGP Sirro ni mtulivu wa na ni mtu anayetafakari maamuzi yake kwa kutafakari bila kujali presha au maagizo ya kisiasa,” Askofu Mwamalanga alisema.Alimuelezea IGP Sirro kuwa ni kiongozi ambaye anawashirikisha wafanyakazi wenzake na wananchi kwa ujumla ili kuleta amani kazi ambayo huifanya kwa weledi.Ameongeza kuwa kiongozi huyo wa juu katika Jeshi la Polisi ni mtu mwenye kuthubutu hasa katika vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya na ujambazi.
“Nakumbuka Kamanda Sirro ni polisi wa kwanza kupata tuzo katika kufanikiwa kudhibiti majambazi,”alisema Askofu Mwamalanga. Kiongozi huyo wa dini ametoa ushauri kwa IGP Mpya kushughulika maslahi ya askari, vitenda kazi katika jeshi la polisi na kurudisha uhusiano mwema kati ya Jeshi la Polisi na raia wema ambao amesema wanafikia takribani asilimia 99.
Aidha, Askofu Mwamalanga ameshauri kuwa IGP aelekeze zaidi nguvu katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, Dar es Salaam, Morogoro, Tanga na Kagera. Ameitaja mikoa mingine kuwa ni Mwanza, Arusha, Kigoma, Dodoma, Pemba na Mara, mikoa ambayo ameitaja kuwa iko kwenye hatari ya vitendo vya uhalifu.
Kamanda Sirro ameapishwa Siku ya Jumatatu Ikulu jijini Dar es Salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Baada ya kuapishwa, IGP Saimon Sirro alikula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma. Kabla ya Uteuzi huo, Kamanda Sirro ambaye sasa in IGP akichukuwa nafasi aliyokuwa nayo Kamanda Ernest Mangu, alikuwa Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam.