Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Ferguson: Manchester United wanaimarika chini ya Mourinho ila wamekosa bahati

Klabu ya Manchester United inaendelea kuimarika chini ya kocha Jose Mourinho na ‘ni bahati tu wamekosa’ lakini wangekuwa wakikabiliana vilivyo na Chelsea, amesema meneja wa zamani Sir Alex Ferguson.

Ferguson ambaye ana umri wa miaka 75, alistaafu kazi ya ukocha mwaka 2013, lakini bado ana uhusiano wa karibu na klabu hiyo ya Old Trafford kwani huhudhuria michezo yao mingi
“Nafikiri Mourinho amefanya kazi kubwa,” amesema Ferguson katika mahojiano na BBC Sports.
Ferguson pia alielezea kwa nini rekodi ya ufungaji magoli ya mshambuliaji wa Manchester united Wayne rooney haitavunjwa na mchezaji yoyote yule karibuni.
Jose Mourinho anakuwa ni kocha wa tatu kuiongoza klabu ya Manchester United tangu Ferguson alivyo staafu, alipochukua nafasi ya Louis van Gaal mwezi Mei.