MAUAJI YA KIKATILI WILAYANI KYELA MKOA WA MBEYA
KYELA 10/04/2016
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Samsoni Mwandembwa(64)mkazi wa kitongoji cha mpunguti kijiji cha mpunguti kata ya makwale amekutwa ameuawa kwa kunyongwa na kutupwa kwenye dimbwi la maji katika kitongoji cha katete kijijini hapo.
Akizungumzia tukio hilo afisa mtendaji wa kijiji hicho Eliki Gwakisa amesema asubuhi ya jumamosi amefika katika eneo la tukio na kuwakuta wananchi huku mwili wa marehemu ukiwa ndani ya dimbwi la maji na baadhi ya vitu vya marehemu vikiwa mbali na mwili huo.
Mke wa marehemu Samsoni na mtoto wake Brayton wamezungumza na masoud maulidi na kueleza hali halisi ya marehemu alivyoaga kabla hajafikwa na umauti kisha kutupwa ndani ya maji.
Kwa upande wa mashuhuda kijijini hapo wamesikitishwa na kitendo kilichotokea na kuliomba jeshi la police kufanya uchunguzi wa tukio hilo na kuwabaini waliofanya mauaji hayo ya kinyama na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Kwa upande wa jeshi la polisi wilayani hapa limekiri kutokea kwa tukio hilo na kuiasa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani madhara yake ni makubwa ndani ya jamii huku kamanda wa polisi mkoa wa mbeya ahmedi Msangi akisema bado hajapokea taarifa ya tukio hilo. Itakumbukwa kuwa tukio hili ni mwendelezo wa matukio ya kutisha ndani ya wilaya ya kyela kwani mpaka sasa ni majuma matatu tangu kutokee mkasa wa kutisha wa watu watatu kunyongwa na kisha kuchomwa moto ndani ya nyumba ya kulala wageni ya Mexiko kyela mjini.