Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Video: Dawa nyingine yakuongeza nguvu kiume yafungiwa ‘Wanaume wengi ndio wanatumia’

 


Baraza la Tiba Asili na Tiba mbadala limepiga marufuku uingizaji, usambazaji, uuzaji na utumiaji wa kinywaji cha kuongeza nguvu kiitwacho AKAYABAGU baada ya kufanya uchunguzi na kugundua kuwa kinywaji hicho hakijawahi kusajiliwa na Baraza hilo Nchini.

Taarifa ya Baraza hilo imesema pia limegundua kuwa kimechanganywa na dawa ya kisasa aina ya sildenafil (Viagra majina mengine Erecto ama Vega) jambo ambalo ni kinyume cha sheria hivyo Watumiaji wamedanganywa na Wahusika ambapo kwa kitendo cha kuchanganywa na Sildenafil (Viagra) kinywaji hiko sio tena cha tiba asili bali ni kinywaji chenye viagra.