Physio wa Chile ametoa taarifa za jeraha la Sanchez nje muda gani
Mshambuliaji wa kimataifa wa Chile anayekipiga katika club ya Man United Alex Sanchez bado anaendelea kuwa na wakati mgumu katika kipindi hiki akiwa na Man United, Sanchez anaingia katika wakati mgumu kufuatia kupata majeraha yatakayomuweka nje ya uwanja kwa mara nyingine tena.
Sanchez siku ya Jumamosi ya February 2 2019 alikuwa sehemu ya kikosi cha Man United kilichocheza dhidi ya Southampton na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-2 lakini alicheza game hiyo kwa dakika 52 na kutolewa kutokana na kuumia goti katika mchezo huo na nafasi yake kuchukuliwa na Dalot.