Neymar asema yuko fiti kucheza fainali za Kombe la Dunia
Mshambuliaji nyota wa Brazil, Neymar Jr amesema yuko fiti kucheza
fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kuanza Juni 14 nchini Russia
bila kikwazo chochote.
Neymar ametoa kauli hiyo muda mfupi, baada ya timu hiyo kuweka kambi jijini London Uingereza kujiandaa kwa fainali hizo.
Neymar amesema ana uhakika wa kucheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Uswis Juni 17. “Niko tayari kucheza, hakuna kitu cha kunizuia,” alisema mchezaji huyo ambaye hajacheza muda mrefu kutokana na jeraha la kifundo cha mguu.

Hata hivyo, benchi la ufundi limejaribu kupunguza presha kwa nyota huyo
kwa kuwa anahitaji muda kurejea katika kiwango bora tayari kwa fainali
hizo.