Majibu ya Serikali kuhusu kuwabagua wanafunzi kwenye mikopo
Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia Willium Ole Nasha imetolea ufafanuzi kuhusu
suala la kutowapa mikopo wa elimu ya juu wanafunzi waliosoma katika
shule binafsi maamuzi yaliyoitwa kuwa ni yakibaguzi. Ole Nasha ametolea
ufafanuzi huo wakati akijibu swali la Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea.