Header Ads

PropellerAds

Breaking News

PSG imempa Cavani ofa ya euro Milioni 1 penalti apige Neymar, amekataa

Mzozo uliotokea baina ya wachezaji wawili wa Paris Saint-Germain, Edinson Cavani na mchezaji-mwenza Neymar wa kugombea kupiga penalti umeingia katika sura mpya baada ya staa huyo wa Uruguay kukataa euro Milioni Moja ili amuachie majukumu ya kupiga penalti staa wa Brazil, kwa mujibu wa ripoti nchini Uhispania.

Gazeti la El Pais la Uhispania, limedai kuwa Cavani alipewa ofa ya malipo, ambayo yatakuwa kama bonus endapo atamaliza kama mfungaji kinara wa klabu hiyo msimu kwenye Ligue 1, lakini mshambuliaji huyo amekataa.

Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi, wiki iliyopita alikuwa na kazi kubwa kuzungumza na Cavani na wawakilishi wake ili kufikia makubaliano kufuatia tendo la aibu lililotokea wakati wa mchezo wao dhidi ya Lyon September 18, 2017 ambapo walishinda mabao 2-0.

El Pais imesema kuwa, PSG ingali inatafuta suluhu baina ya mastaa hao wawili huku ikielezwa wachezaji wengi wa klabu hiyo wakitaka jukumu la penalti apewe Cavani.