Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hemed Phd amesema wakati anakuwa
alikuwa mzuri kama mtoto wa kike, kitendo ambacho kilimuingiza kwenye
matatizo mengi ikiwemo kufukuzwa shule.
Akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio,
Hemedi amesema muonekano wake wenye kuvutia, ulisababisha awe na
mahusiano na mke wa mwalimu na kupelekea kufukuzwa shule aliyokuwa
akisoma.
"Unajua kabla sijaanza kukua na kutoka zile chunusi chunusi mi nilikuwa
kama demu, nilikuwa nahenyesha sana walimu wa kike walikuwa wananikubali
sana, bebe zilikuwa zinaelewa sana, lakini kutokana na umri na
mazingira nikawa navunga, nishapata kesi mimi nikiwa sekondari kidato
cha pili kutembea na mke wa mwalimu nikafukuzwa shule, lakini yote ni
sehemu ya maisha tunapita", amesema Hemedi.
Hemedi kwa sasa anadai mambo hayo ameacha kwa sababu ameshakuwa mtu
mzima na yuko na familia, ambapo ana mke na mtoto mmoja. Lakini pia
msanii huyo ameichia kazi yake mpya sasa inayojulikana kwa jila la
'Mkimbie'.
Hemedi Phd afunguka kilichomfanya afukuzwe shule
Reviewed by mwabusila
on
9/19/2017 09:13:00 PM
Rating: 5