SOMA KWA MAPANA KWANINI MHE.DK.JOHN MAGUFULI ALIVYO ONDOA SHEREHE ZA UHURU
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli
ameagiza siku ya sikukuu ya Uhuru, 9 December hakutakua na sherehe za kitaifa
na badala yake watu watatumia siku hiyo kufanya usafi katika maeneo yao.
Maamuzi haya yamekuja siku chache baada ya Dk.Magufuli kutoa
tena agizo la fedha zaidi ya milioni 250 ambazo zilikuwa zitumike kwenye
sherehe za ufunguzi wa Bunge, Dodoma kuelekezwa kwenye ununuzi wa vitanda vya
wagonjwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Rais amechukua maamuzi hayo kutokana na kukerwa na ugonjwa
wa kipindupindu ambao tayari umepoteza maisha ya watu na bado umeendea kukumba
maeneo mbalimbali nchini.
Kwa niaba ya Rais, Katibu Mkuu kiongozi Ombeni Sefue baada
ya kufanya ziara katika hospitali ya muhimbili alisema Rais ameagiza kuwa siku
hiyo hakutakuwa na sherehe zozote za kitaifa na badala yake wananchi wataitumia
kufanya usafi katika maeneo yao.
“Rais amesema suala la kuwepo ugonjwa Kipindupindu
halikubaliki, jambo hili limemkera sana, tunasherehekea miaka 54 ya uhuru
lakini bado kipindupindu kinatusumbua sana, amesema kama Watanzania lazima
tulishughulikie, haiwezekani akija mgeni kama Obama tunafanya usafi lakini
akiondoka tunaendelea kuwa wachafu, ameamua tarehe 9 December siku ya uhuru
hakutakuwa na sherehe yoyote badala yake watu wakasafishe maeneo yao”..Ombeni
Sefue.Chanzo cha habari millardayo.com